WEWE NI MGENI? KARIBU SANA, BOFYA HAPA UJUE ZAIDI.



Kama ulitusikia mtandaoni, kwa ndugu, jamaa au rafiki, basi hujakosea kabisa. Vuta kiti, kaa tukupashe habari.

Kama uko hapa bila shaka wewe ni mpenzi, mdau, au mfuatiliaji wa soka tena hasa soka la Tanzania. Kama ni hivyo uko sehemu sahihi.

Habari ni kwamba kwa mchango wa wadau kadhaa wa soka Tanzania Luqman Kabange amefanikiwa kuanzisha gazeti mtandao la kwanza nchi. Kama unapenda vipaji, unapenda soka, na unapenda kuujua mchezo wenyewe LigiKuu_Xtra ni sehemu sahihi kwako.

Ni dhahihiri kuwa kila mwana michezo mwenye mahaba na mchezo husika huhitaji kujua na kupata taarifa kiundani. Hapa hilo ndilo dhumuni letu kuu. LigiKuu_Xtra ni uwanda wa kimichezo uliotandaa na kutondoka katika ligi kuu soka Tanzania.


Kwa nini LigiKuu_Xtra.

Soka ni tamu, na kama unalipenda kwa dhati basi ni tamu zaidi. Tungo za maneno yenye rejea zenye ubunifu wa fikra zinapatikana hapa. Hapa utapata maono, maoni, mijadala na uchambuzi wa kina juu ya ligi namba sita kwa ubora barani Afrika.

LigiKuu_Xtra itakupatia:
  1. Uchambuzi wa kina kabla ya mechi: tutatumia maneno ya makocha, wachezaji na wataalumu wengine kukujuza ni kipi cha kutegemea na ni maeneo gani ya kutupia jicho. Hayo yataambatana na upembuzi juu ya mifanano katika ishara kueleza ni matukio yana uwezekano mkubwa wa kutokea.
  2. Uchambuzi wa kina baada ya mechi: tutatanabahisha mipango ya kila timu kiwanjani na kwa kurejea hadidu zetu tutaeleza mipango ya kila timu na  utekelezwaji wake kiwanjani.
  3.  Uvumbuzi wa vipaji vinavyochipukia: kama kuna kijana anaonesha mwanga na ametokea kukubalika na walimu wake sisi tupo kukujuza sifa zake, daraja la uwezo wake na kama anaweza kufanya ayafanyayo kwenye klabu nyingine.
  4. Ripoti kamili ya vipaji chipukizi: kila kijana atakayefikia macho yetu LigiKuu_Xtra ipo kukupa taarifa kamili juu ya uwezo wake.
Hayo yote utayapata katika lugha adhwimu ya kiswahili yakambatana na vipande vya video na picha ili kutoa maelezo bayana.

Sasa wajua, karibu, jiunge nasi.

LigiKuu_Xtra itakupatia nakala moja ya gazeti kila wiki. Jua kuwa hapa ni kitovu cha weledi na uaminifu, tunajikita kuhakikisha wasomaji wetu wanapata kilicho bora zaidi. Furaha yetu ni kuridhika kwako na tutafanya chochote kufanikisha hilo.

LigiKuu_Xtra inatoa huduma za ushauri, uvumbuzi wa vipaji na uchambuzi wa video. Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kurasa zetu za mitandao ya jamii kwa jina la @LigKuu_Xtra.

Maoni

  1. Kwa maneno hapo juu matarajio ni makubwa kwenye coverage ya ligi kuu kila la heri

    JibuFuta

Chapisha Maoni